Kukua katika Imani

Mapenzi ya Mungu ni kila muumini, mmoja mmoja, akue na kufika katika kiwango cha imani, nguvu na neema aliyokuwa-nayo BWANA wetu Yesu Kristo. Ndio maana “… alitoa wengine kuwa Mitume, Manabii, Wachungaji, Wainjilisti na Waalimu, kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu [wote], ili mwili wa Kristo [Kanisa] ujengwe, hata na sisi sote [kama waumini], tukue na kufika katika kimo cha utimilifu wa Kristo, ili tusiwe watoto wachanga … ili tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa-tupwa huku na huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa elimu, kwa hila za watu [na] kwa ujanja, … lakini tuishike kweli katika upendo na kukua, hata tumfikie Yeye, katika yote, Yeye aliye kichwa, yaani Kristo ” (Efeso 4:11-15).

Lakini watoto wa Mungu wengi wamekuwa wavivu katika kumtafuta Mungu na kukua katika imani (Waenrani 5:11-14), ndio maana BWANA Yesu anawagombeza sana wanafunzi wake kwa kushindwa kumtoa pepo (Mathayo 17:14-21). Hali hiyo inawahusu wanafunzi wengi wa Yesu wa leo. Hali hiyo inamhuzunisha sana Yesu mpaka leo. Katika semina hii, tulijifunza namna ya kukua katika imani, neema na nguvu za Mungu, ili tusitawaliwe na mazingira, bali sisi ndio tuyatawale mazingira yote kwa ushindi na mafanikio. Unaweza kupata mafundisho haya kwa kuweka ‘order’ katika duka la mtandanoni, sehemu ya chini ya ukurasa huu. Jina la CD/DVD hii ni Jifunze Vita Kiroho. Nakutakia neema ya Mungu ya kukua na kuongezeka katika imani, neema na nguvu (Rum 1:17, Yoh 1:17, Zab 84:1-7 na 2Kor 3:18).